MAO.DAFU
2023-04-16 11:07阅读:
ULIMWENGU WA KISWAHILI 斯瓦希里语世界
THE SWAHILI WORLD
聊 斋
志
异
选
MASIMULIZI TEULE YA AJABU KUTOKA KWENYE UKUMBI WA
SOGA
SELECTED STRANGE TALES FROM CHAT STUDIO
Mwandishi: Pu Songling
Mchapishaji: Shirika la Uchapishaji wa Umma wa
Jilin
2021年3月由深圳市碧兰星印务有限公司印制
DIBAJI
Pu Songling (1640 – 1715)
alikuwa mwandishi mashuhuri wa fasihi ya kale ya China.
Ali
kuwa mwenyeji wa Kijiji chaPujia, Mji wa Zichuan, jimboni
Shandong.alizaliwa katika ukoo wa kikabaila uliokuwa ukitopea na
kuzorota. Alipokuwa na umri wa miaka 19 alipata shahada ya kwanza
na sifa yake ilikuwa kubwa, lakini hakufaulu maishani katika
mitihani ya ngazi ya juu iliyofuata, ijapokuwa alijaribu mara
nyingi sana. Kwa kuwa hali ya maisha ilikuwa duni, aliwahi kufanya
kazi ya utumishi kwa Mkuu wa Wilaya ya Baoying kwa mwaka mmoja na
kufanya kazi ya ualimu katika koo za makabaila wakubwa kwa miaka
mingi. Maisha yake ya ufukara yalimfanya afahamu ugumu na uchungu
wa makabwela; kutokufaulu kwake katika mitihani kulimfanya agundue
kasoro za mfumo wa mitihani ya kifalme; kazi za utumishi
alizozifanya chini ya mkuu wa wilaya zilimfanya ajionee upotovu wa
uwanja wa maofisa. Hivyo alianza kujenga chuki na jamii siku baada
ya siku na akawa na mawazo ya kutumaini kuiondolea matatizo jamii
hiyo ambayo ilifunikwa kwa giza totoro.
Katika kitabu cha Masimulizi ya Ajabu Kutoka
Kwenye Ukumbi wa Soga ingawa mwandishi alieleza habari
nyingi kuhusu mashetani na mbweha lakini kwa kweli hadithi hizi
zilisheheni simanzi na hasira za Pu Songling kwa jamii
ambazo zilijikusanya kifuani mwake. Kitabu hiki kilieleza maisha,
mila na mawazo ya watu walioishi katika China ya kimwinyi.
Kilifichua uovu na uasherati wa wafalme, maofisa na makabaila
wakubwa,hali kadhalika kilieleza umaskini na shida nyingine za watu
duni; kilikejeli kasoro za mfumo wa mitihani ya kifalme ya miaka
iliyopita; kilisuta ubaya wa mfumo wa ndoa ya kimwinyi na vilevile
kilisifu juhudi za wavulana na wasichana katika kujipatia maisha
mema.
Mwandishi alichukua hadithi za mapokeo kama msingi wa
utungaji wake, na alifanikiwa kutunga hadithi nyingi nzuri.
Alikusanya, kuratibu na kutunga hadithi hizi za ajabu siyo kwa
sababu aliamini ushirikina, bali kwa kuwa watawala wa Enzi ya Qing
waliendesha siasa ya kikatili kuhusu utamaduni. Watu waliothubutu
kukosoa siasa za falme aghalabu waliuawa au kutiwa gerezani. Kwa
ajili ya kuepukana na majanga, na kuweza kueneza hadithi zake, Pu
Songling alitumia njia ya kuzungumzia habari za mashetani na mbweha
kumithilisha hali ilivyokuwa katika miaka ya zama
zake.
Kitabu hiki ni kimojawapo kati ya vitabu maarufu vya
hadithi katika historia ya fasihi ya China. Pu Songling alianza
kutunga kitabu hiki tangu alipokuwa na umri wa miaka 20 hivi, na
alimaliza kukitunga kimsingi alipokuwa na umri wa miaka 50. Kwa
ujumla kina hadithi 490 na zaidi. Miaka 200 imepita tangu kitabu
hiki kuandikwa. Kitabu hiki kimewavutia na kuwafurahisha wasomaji.
Katika miaka 100 iliyopita, baadhi ya hadithi za kitabuhiki
zimetafsiriwa katika lugha za kigeni zaidi ya 20 na kinajulikana
sana katika uwanja wa fasihi ya ulimwengu.
Kwa kutumia fursa hii tunashukuru mtaalamu wa Kiswahili
PILI MWINYI wa Tanzania aliyepitia muswada mzima wa tafsiri na
kutoa maoni yake ya kusahihisha makosa na kuboresha muswada huo.
Zaidi ya hayo, tunatoa shukrani kwa mchapishaji CHANG
HONG(常 宏),
makamu wa mhariri mkuu ZHAO YAN(赵
岩), mhariri DING HAO(丁 昊),
wachoraji picha GAO ZHENXIANG(高振翔), WANG YAN(汪
艳), PENG TINGYAO(彭婷遥) wa
Shirika la Uchapishaji wa Umma wa Jilin
(吉林人民出版社)na watu wote wengine waliowahi
kutusaidia mnamo muda wo wote wa uchapishaji wa vitabu
hivyo.
ULIMWENGU WA KISWAHILI
斯瓦希里语世界 THE SWAHILI
WORLD
MASIMULIZI TEULE YA AJABU KUTOKA KWENYE UKUMBI WA
SOGA
聊斋志异选
SELECTED STRANGE TALES FROM CHAT
STUDIO
Mwandishi: Pu Songling
MAO DAFU
Hapo kale, paliondokea mganga mmoja
aliyeitwa Mao
Dafu ambaye
alibobea katika
kutibu majipu huko Safu ya
Milima
Taihang.
Siku
moja,
aliporejea
kwake baada ya kutibu
wagonjwa,
a1imkuta
mbwamwitu
mmoja,ambaye alileta
kifurushimdomoni,
kisha
akachuchumaakando ya
barabara.
Mao alikiokota
kifurushi hicho. Baada ya
kukifungua aliona mapambo
kadhaa yaliyotengenezwa kwadhahabu.
Wakati Mao
alipokuwa
akipigwa na butwaa,
alimwona
mbwamwitu alikuja
mbele yake, akarukaruka
na kuivuta kanzu yake mara kadhaa kwa mdomo,
halafuakaondoka
polepole. Mao
hakutiliamaanani,
aliendelea
na safari
yake. Mbwamwitu
alirudi akavuta kanzu
yake tena.Mao aliona
mbwamwitu huyu hana nia
mbayaakamfuata. Walitembea kwa
muda,wakaingia katika
pango moja kubwa. Mao
alimwona
mbwamwitu
mwingine ambaye
alikuwa anaugua na amelala
ardhini.
Mao alipoangalia kwa uangalifu
aligundua
jipu moja kubwa
kwenye utosi wake
ambalo limeozana
ndani ya jipu hilo
mna
mafunza
wengi. Alifahamu
madhumuni yao,
akakwanguavitu vichafu vilivomo ndani ya
jipu, akalisafisha na
kupaka dawa,
akaenda zake. Wakati
huo, giza
ilizidi nambwamwitu alimsindikiza nyuma
yake. Walipotembea kiasi cha
kilomita mbili hivi
waliwakuta
mbwamwitu wengine
kadhaa,nao walitaka
kumshambulia
Mao huku
wakilialia.Mao alihofu
kupita kiasi. Mbwamwitu yule
aliyemsindikiza
alipiga mbio
chapuchapu na kuingia
katika kundi
1a mbwamwitu hao,
akaonekana kama anawaambia
maneno fulani. Dakika
chache tu baadaye,mbwamwitu
wote pamoja na yule aliyemsindikiza
Mao wakaenda
zao. Mao
pia
aliendelea na safari yake ya
kurejea nyumbani.
Chanzo cha jambo hilo
hasakilikuwa hivi:
Katika wilayahiyo
palikuwa na
mfanyabiashara mmoja
aitwaye
Ning
Tai
ambaye aliuza mapambo
ya dhahabu na fedha. Siku moja,
aliuawa na
jambazi alipokuwa
akisafiri njiani.
Jambazi huyo hakuachaalama
yoyote ya kuweza kujulisha
amekwenda
wapi.
Wakati Mao
alipouza
mapambo hayo
ya dhahabu, sadfaalionwa na
mke wa
Ning.
Basi mke wa Ning
alimburura
Mao hadi
mahakamani. Mao alieleza jinsi
alivyoyapata
mapambo hayo, lakini hakimu
hakusadiki,
akaamuru apigwe kwa ubao.
Mao
hakuwa na
njia ya kujitetea,
akapigwa bure. Iliyobaki ilikuwa amwombe hakimu kutoa kibali
iliaende kuuliza wale mbwamwitu. Hakimu alituma watumishi wawili wa
mahakamaniwafuatane naye, walifika mapango ya mbwamwitu moja kwa
moja. Walikutambwamwitu hawapo.
Walisubirimpaka wakati wa
magharibi,
mbwamwitu walikuwa bado hawajarejea,
basihao watatu
waliamua kurejea.
Njiani walipofika nusu ya safari,
waliwakuta mbwamwitu
wawili ambao kati yao mmoja ana kovu
utosini.Mao
aliwatambua,akawasalimu
kwa heshima na
kusema,”Majuzi nilipata tuzo
yenu lakini leo hiinimekamatwa kwa
sababu ya tuzo hiyona
kuzuliwa hatia. Leo msipowafahamisha
watumishi hawa
wawili jambo hilo,
nitapigwakwa
ubao mpaka
kufa baada ya kurejea
mahakamani.”
Mbwamwitu walipomwona
Mao amefungwa
kwa kamba
walivamia watumishi fulifuli.
Watumishi hao
wawili walichomoapanga wakakabiliana nao.
Mbwamwitu waligusa ardhi
kwamdomo, wakabweka kwa sauti
yajuu. Baada ya
kulia mara mbili
tatu, kiasi cha mbwamwitu mia wa
milimani
walijikusanya
huko,wakawazunga Mao na
watumishi, nao waliogopamno.
Mbwamwitu
walishindana
kumfungulia
Mao fungato.
Baada ya kitambo, watumishi wakafahamu
nia yambwamwitu, basi walifungua Mao na mara tu mbwamwitu wote
wakaenda zao. Baada yakurejea mahakamani, wale
watumishiwawili
walimwelezea
hakimu
waliyoyaona.Hakimu
alistaajabu
bali
hakumwachia huru Mao.
Siku
chachebaadaye,hakimu huyo alikwenda
nje kusafiri. Mbwamwitu
mmoja alisimamabarabarani na huku
akiuma kwa meno
kiatu kibovu. hakimu huyo
alipita na mbwamwitu
alipigambio na kumpita hakimu kwa
kasi hadi mbele
yake,akakiweka kile
kiatu kibovu
katikati yabarabara. Hakimu
alimwamuru
mfuasi wake
achukue kile
kiatu, baada
yahapo, mbwamwitu akaenda
zake.
Aliporejea
mahakamani hakimu
alimtuma mfuasiwake aende
kisirisiri
kutafuta mwenye kiatu hicho.
Mtu mmoja alisema
kuwa
katika kijiji
kimoja palikuwa
na mtu mmoja aitwaye
Cong
Xin ambaye aliwahi
kufukuzwa na mbwamwitu
wawili. Mmoja
wao aliwahi kukiuma
mdomoni kiatu
kibovu cha
Xin na
kuondoka.
Watumishi wa mahakama
walikwenda kumwita Cong Xinili
aje
kuthibitisha jambo
hilo,kumbe kiatu
kibovu hicho kweli ni
chake,hivyo
walishuku kwamba ni
Xin
aliyemwua
Ning.
Hakimu
alimhojiXin,
akafahamu kweli
Xinalikuwa mwuaji. Chanzo cha
jambo hilo kilikuwa
hivi:Xin alimwua
Ning. Baada ya kumwua,
alipokonyakiasi kikubwa cha fedha,
lakini hakudiriki kupekuapekua zaidi, hivyo
hakuona
mapambo
yale ya dhahabu
yaliyofichwa
chini ya
mavazi, na
baadayemapambo hayo ya dhahabu yakachukuliwa na
mbwamwitu.
Hapo
zamani,palikuwa
na mkunga mmoja. Siku moja
alipokuwa akirudi nyumbani kwakealimkuta
mbwamwitu njiani. Mbwamwitu huyo alimzuia
nakuvuta nguo yake kama kwamba
anataka
kumvutakwenda
mahali fulani,
mkunga huyo
akamfuata,halafu
alimwona
mbwamwitu jike
ambaye alishindwa kujifungua.
Mkunga huyo
alimsaidia kwa
kumkanda. Baada ya
kufaulu kumzalisha
mbwamwitu jike, mbwamwitu yule dume alimwachamkunga kurejea
nyumbani. Siku ya pili, kwa ajili ya kumshukuru, yule
mbwamwitu dume
alimpelekea nyama ya paa na kuiweka nyumbani
mwake.Kutokana na
hadithi hizi
tunaweza kujua kwamba mambo kama
hayo yaliwahi kutokea,bali si mara
moja tu.